2 Oktoba 2025 - 13:17
Source: ABNA
Kuanza Kutekelezwa kwa Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kimkakati Kati ya Iran na Urusi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetangaza kuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Kimkakati kati ya Urusi na Iran unaanza kutekelezwa rasmi kuanzia leo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s.) - ABNA - Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kimkakati kati ya Shirikisho la Urusi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambao ulitiwa saini huko Moscow tarehe 27 Dey 1403 (Januari 2025) na Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Masoud Pezeshkian, rasmi umeingia katika awamu ya utekelezaji kuanzia leo, 10 Mehr 1404 (Oktoba 2, 2025).

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, "Mkataba huu unachukuliwa kama hatua muhimu katika historia ya mahusiano ya pande mbili kati ya Urusi na Iran na umeimarisha kiwango cha mahusiano ya nchi hizo mbili hadi hatua mpya ya ushirikiano wa kina wa kimkakati. Hati hii inaweka miongozo muhimu ya ushirikiano wa muda mrefu katika maeneo yote ya kipaumbele."

Kulingana na mkataba huu, nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano wao katika medani ya kimataifa na zitakuwa na uratibu wa karibu katika mfumo wa mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuunda utaratibu wa dunia wa pande nyingi. Pia, juhudi za pamoja zimepangwa ili kuimarisha utulivu na usalama wa kikanda na kukabiliana na changamoto na vitisho vya pamoja.

Mwishoni mwa taarifa hiyo imeelezwa: Makubaliano haya yanaonyesha chaguo la kimkakati la viongozi wakuu wa kisiasa wa nchi 2 kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ujirani mwema, ambao unaendana na maslahi ya msingi ya mataifa ya Iran na Urusi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha